Yafahamu mambo 10 yanayoweza kuharibu Ubongo wa binadamu

Ubongo ndio ikulu yako, huratibu na kusimamia kazi zote za mwili wako ikiwa ni pamoja na kuongea, kufikiri na kuvumbua vitu vipya. Watu wengi wanafanikiwa kiuchumi kwa kutumia vizuri ubongo wao ili uwaletee maendeleo.
Kwa kutambua umuhimu wa ubongo katika maisha yetu wasomaji wa FikraPevu hatuna budi kutambua mazoea kumi yanayoharibu ubongo wetu bila ya sisi kujua.
Kukosa mlo wa asubuhi
Watu wasio pata kifungua kinywa chenye lishe aina ya wanga na protini wanaweza kupatwa na upungufu wa sukari kwenye damu. Hali hii inasababisha ubongo kutopata virutubisho vya kutosha na kufanya ubongo kuanza kuharibika. Aidha, kukosa mlo wa asubuhi kunasababisha matatizo mengi ya kiafya yakiwa pamoja na kupanda kwa shinikizo la damu, kunenepa kupita kiasi na mpangilio mbovu wa mafuta katika damu.
Kukosa mlo wa asubuhi kunaufanya mwili ukae katika hali ya mkazo kwa kukaa njaa muda mrefu kwa sababu inapokuwa asubuhi unakuwa na shughuli nyingi na mwili unahitaji nguvu za kutosha, hivyo kukosa kifungua kinywa kizito kunaharibu utendaji wa kimetaboliki wa mwili na kusababisha hali za hatari kwa afya ya mtu.
Kwa kutambua umuhimu wa ubongo katika maisha yetu wasomaji wa FikraPevu hatuna budi kutambua mazoea kumi yanayoharibu ubongo wetu bila ya sisi kujua.
Kukosa mlo wa asubuhi
Watu wasio pata kifungua kinywa chenye lishe aina ya wanga na protini wanaweza kupatwa na upungufu wa sukari kwenye damu. Hali hii inasababisha ubongo kutopata virutubisho vya kutosha na kufanya ubongo kuanza kuharibika. Aidha, kukosa mlo wa asubuhi kunasababisha matatizo mengi ya kiafya yakiwa pamoja na kupanda kwa shinikizo la damu, kunenepa kupita kiasi na mpangilio mbovu wa mafuta katika damu.
Kukosa mlo wa asubuhi kunaufanya mwili ukae katika hali ya mkazo kwa kukaa njaa muda mrefu kwa sababu inapokuwa asubuhi unakuwa na shughuli nyingi na mwili unahitaji nguvu za kutosha, hivyo kukosa kifungua kinywa kizito kunaharibu utendaji wa kimetaboliki wa mwili na kusababisha hali za hatari kwa afya ya mtu.
Kula kupita kiasi
Mwili hutumia kalori zinazopatikana katika vyakula, kwa ajili ya
utendaji wa misuli, ogani, tishu na seli. Kila mtu anahitaji kiwango
chake cha kalori kwa kutegemea umri, jinsia, kimo, uzito wake wa sasa na
aina ya kazi anayofanya. Kula kupita kiasi kunasababisha ateri za
ubongo (mishipa ya damu iliyosheheni hewa ya oksijeni ambayo hutoa damu
kwenye moyo na kuisafirisha kwenye ubongo) kuwa migumu hadi kupelekea
kupungua nguvu ya akili.
Aidha, kalori za ziada huhifadhiwa kama mafuta kwa matumizi ya baadae
ingawa watu wengi hawatumii kalori hizo za ziada na kusababisha unene na
kuzidi uzito.
Uvutaji tumbaku
Uvutaji husababisha kusinyaa kwa ubongo kitu kinachoweza sababisha
ugonjwa wa Alzheimer/Alzeima pia hujulikana kama udhaifu wa kiakili
utokanao na uzee wa aina ya Alzeima. Ugonjwa huu usiotibika husababisha
kupoteza kumbukumbu haraka zaidi. Wanasayansi wanadai kuna zaidi ya
mchanganyiko wa kemikali 4,000 katika sigara.
Kemikali za aina nyingi zina athari mbaya katika seli zetu, baadhi
zinasababisha saratani na kufa kwa seli, hivyo uvutaji sigara unaweza
kuua seli za ubongo pia.
Matumizi ya sukari kwa wingi
Ulaji wa sukari kwa wingi mfano vyakula vyenye sukari kama soda na
juisi za viwandani unaingilia ufyonzaji wa protini na virutubisho
vingine na kusababisha utapiamlo unaoweza haribu ukuaji wa ubongo. Ulaji
wa sukari kwa wingi katika mlo wako hakuta kuongezea tu uzito, bali
utasababisha athari hasi kwenye afya ya mwili wako.
Mfumo wa ulinzi wa mwili wako ndio njia muhimu ya kuulinda mwili wa
binadamu. Kutumia sukari kwa wingi kuna athiri utendaji wa mfumo huu na
kupunguza uwezo wa kupambana na virusi, bakteria na vimelea vingine
ambavyo vinaweza kuathiri ubongo pia.
Kuufanyisha ubongo kazi wakati unaumwa
Ubongo ni moja ya ogani tata ya mwanadamu ikiwa na uwezo mdogo wa
kujifanyiza. Ubongo ni rahisi kuathiriwa na ugonjwa. Kupoteza au
kuharibika kwa mtandao wa seli za ubongo kunaweza sababisha athari kubwa
katika ubongo hasa ukilazimisha ubongo kufanya kazi wakati unaumwa.
Kufanya kazi sana au kusoma sana huku unaumwa kunaweza kupunguza ufanisi
wa ubongo pamoja na kuharibu ubongo.
Uchafuzi wa hewa
Ubongo ndio kiungo kikubwa kinachotumia hewa ya oksijeni katika mwili
wako. Kuvuta hewa chafu kunapunguza usambazaji wa oksijeni katika ubongo
na kusababisha kupungua kwa ufanisi wa ubongo. Kukaa sehemu yenye hewa
nzuri kama mlimani au ufukwe mzuri kunaweza kupumzisha ubongo na
kuuimarisha.
Kutosinzia vya kutosha
Kusinzia kunaruhusu ubongo kupumzika. Kujinyima usingizi wa kutosha kwa
muda mrefu kutaongeza kasi ya kufa kwa seli za ubongo. Watoto wachanga
wa chini ya umri wa mwaka mmoja wanapaswa kulala kwa kati ya saa 16 na
18 kwa siku, wakati wenye umri wa kuanzia mwaka mmoja hadi mitatu
wanahitaji saa 14.
Watoto wenye umri wa miaka mitatu hadi minne wanahitaji kulala walau
kati ya saa 11 na 12, wakati wenye umri wa kwenda shule, kwa maana ya
miaka sita na saba, wanahitaji walau usingizi wa saa 10 kila siku, huku
vijana wenye umri wa balehe na watu wazima wanashauriwa wapate usingizi
wa kati ya saa saba na nane.
Kufunika kichwa wakati umelala
Kulala huku umefunika kichwa mfano kwa wanawake wanaovaa kofia maalumu
ili zisiharibu nywele walizosuka au kutengeneza kunaongeza msongamano wa
hewa chafu ya kabonidioxide (dioksidi ya kaboni) na kupunguza oksijeni kitu kinachoathiri ubongo.
Kukosa fikra chanya
Kuwa na fikra pevu ndio njia bora ya kuufunza ubongo wako, kukosa fikra chanya kunaweza kufanya ubongo kudhorota.
Kuzungumza kwa nadra
Mazungumzo yenye busara yatachochea ufanisi wa ubongo wako. Ni vyema
kutoa dukuduku lako kwa kuzungumza kila mara unapohisi kuwa unalo
kwasababu linaweza kuathiri afya yako kiujumla.
No comments:
Post a Comment