Leonidas Gama ashinda Ubunge Songea, Mabomu yatumika kutawanya wananchi

Kwa mujibu wa Msimamizi Mkuu wa Uchaguzi wa Jimbo hilo, Rafael Kimari, amemtangaza mgombea huyo na kwamba katika kinyang'anyiro hicho kulikuwa na vyama vitatu ambavyo vilisimamisha wagombea kikiwemo chama cha ACT Wazalendo,CCM na Chama Cha Demokrasia (Chadema).
Kimari amekaririwa akimtangaza, Gama, kuwa mshindi kwa kupata kura 40,886 na kufuatiwa na mgombea wa Chadema, Joseph Fuime, aliyepata 37,000 na mgombea wa ACT Wazalendo, Emmanuel Msabila ambaye alipata kura 436.
Aidha, amesema kuwa katika jimbo hilo idadi ya watu waliojiandikisha walikuwa ni wapigakura 127,738. Jimbo hilo lina Kata 21 na kati ya hizo CCM kimefanikiwa kushinda Kata 16 , Chadema kikifanikiwa kushinda Kata 4 na Chama Cha Wananchi CUF kikishinda Kata 1.
Awali kabla ya kutangazwa matokeo hayo ya nafasi ya Ubunge wananchi walijitokeza kwa wingi kwenye viunga vya Halmashauri ya Manispaa ya hiyo ya Songea kwa lengo la kupata matokeo ambayo yalitakiwa kutangazwa majira ya saa tano asubuhi mpaka saa sita mchana kushindikana na kusababisha Jeshi la Polisi kuwataka wananchi waweza kutawanyika na wao kukaidi na kusababisha Polisi kutumia nguvu ya ziada kwa kuwapiga mabomu ya machozi ili kuwatawanya.
Hata hivyo, kuanzia majira ya saa nane mchana, barabara kadhaa za manispaa hiyo zilifungwa na Jeshi la Polisi kutoa amri ya kufunga maduka na biashara zote hali ambayo ilisababisha taharuki kwa wakazi wa Manispaa ya Songea.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma, Mihayo Msikhela, amesema kuwa wafuasi wa Chadema walivumiliwa kwa muda mrefu wakifanya fujo na kuranda randa katikatika ya mji wakishinikiza matokeo yatangazwe bila kufuata utaratibu hali ambayo iliwalazimu askari kutumia mabomu kuwatanya na kupisha kutangazwa kwa matokeo hayo.
Matokeo mengine ya awali ya uchaguzi mkuu.
No comments:
Post a Comment