Sunday, 13 March 2016

Mkutano mkubwa wa hadhara wa kumtambulisha Katibu mkuu CHADEMA Dr Vicent Mashinji -Furahisha Mwanza

Ni Jumapili njema yenye kila aina ya shamrashamra hapa Mwanza.

Jumapili iliyoingia katika historia ambayo usiku wa kuamkia kwake Taifa limeshuhudia Msomi aliyebobea Dr Vicent Mashinji akiukwaa nafasi ya Katibu mkuu wa chama kinachopendwa zaidi nchini CHADEMA.

Freeman Mbowe gwiji wa siasa za Tanzania aliicha dunia mdomo wazi pale alipotamka jina ambalo halikutarajiwa kabisa kuvaa viatu vya Katibu Mkuu.Shangwe nderemo na hoihoi za wajumbe ziliashiria kukubalika kwa mteule huyo wa Mwenyekiti.

Kama ilivyotangazwa awali kijana huyo mwenye miaka 43 na msomi ambaye huenda ndiye msomi kuliko makatibu wakuu wa vyama vyote duniani atapanda jukwaani kutambulishwa kwa umma.

Mkutano wa kumtambulisha Dr Mashinji utafanyika katika viwanja vya Furahisha kuanzia saa 8 mchana na utahudhuriwa na viongozi wote wakuu.

Tutawaletea kila kitakachojiri katika mkutano huo unaotarajiwa kuvunja rekodi ya mikutano jijini Mwanza kwa miaka ya karibuni.

No comments:

Post a Comment